Sauti ya Jogoo. Jifunze sauti ya jogoo na maisha ya wanyama wa nyumbani. Jifunze kuhusu sauti zao, chakula chao, mahali wanapoishi na pia nani ni mlafi kupita wengine. Hadithi imepambwa kwa michoro yenye rangi za kuvutia ya aina ya Tingatinga ili watoto wafurahie wakati wanajifunza. Corona Cermak amezaliwa nchini Tanzania. Ana Shahada (Digrii) ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha London. Kwa sasa, anaishi Brno, Jamuhuri ya Czech na mume wake na watoto wao wawili. Corona ni mwalimu wa Chekechea, shule ambayo inafuata mfumo wa ufundishaji unaomshirikisha mtoto katika mchakato mzima wa kujifunza (Reggio Emilia.) Pia ni mpenzi wa kuandika, kusimulia na kutayarisha hadithi za watoto.